Wednesday, February 12, 2014

CHANGAMOTO HAZINIZUII KUFANYA YANGU KAMA MTOTO WA KIKE-LIL STIGGAR

Katika tasnia ya bongo kumekuwa na changamoto kubwa kwa watoto wa kike kufanya muziki huo na kuweza kufanikiwa hali hii inapelekea wasichana wengi kuogopa kupambana na changamoto hizo na mwisho wanaishia kuwa na ndoto za kuwa wanamuziki au waimbaji pasipokusitimiza ndoto zao. Lakini imekuwa tofauti kigogo kwa msanii Lil Stiggar ambae mbali na kusoma ameamua kujikita katika kiwanda cha muziki na kufanya yake pasipo kuogopa changamoto ambazo anakuwa akikutana nazo katika mazingira ya kazi yake hiyo ya muziki. “Ni kweli kama mtoto wa kike changamoto zinakuwepo lakini kama unakuwa na mipango na umekusudia kufanya kazi unakomaa nazo na mwisho wa siku mambo yanakwenda” Stiggar ameongeza kuwa aina ya changamoto kubwa anayokumbana nayo ni usumbufu kutoka kwa baadhi ya wanaume ambao si waelewa. Nakupa nafasi ya kuitizama Video ya Mkali huyu kutoka pande za Mbeya City.

0 comments:

Post a Comment