Kocha
wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema kuwa hana hofu yoyote na mechi
ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City itakayofanyika
Jumamosi
kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.Simba ambayo awali ilipanga kwenda Mbeya leo, sasa itaondoka kesho Ijumaa kwa usafiri wa ndege.
Logarusic, alisema kwamba anaifahamu Mbeya City na mara nyingi mechi zinazohofiwa ndiyo huwa na matokeo mazuri kwake na kwa klabu nyingine.
Logarusic alisema kwa kifupi kwamba anajua katika hatua ya lala salama hakuna mechi rahisi na kikosi chake kimejiandaa kusaka ushindi.
"Kila mmoja anataka ushindi, tunakwenda kutafuta pointi na tuko tayari kwa changamoto zote," Logarusic alisema kwa kifupi.
0 comments:
Post a Comment