Monday, February 10, 2014

BEN POL KUACHIA UNANICHORA KESHO

Mwanamuziki bora katika Rnb Ben Pol siku ya kesho atatambulisha wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2014 na kutambulisha Album yake inayokwenda kwa jina
la (Ben Pol) ambayo itauzwa kwa njia ya mtandao na itakuwa na nyimbo 20 ndani yake.
Ben Pol amesema wimbo wake wa Unanichora amefanya na mtayarishaji Fundi Samwel na imebeba ujumbe wa mapenzi ndani yake,kwa mwaka huu mkali huyo anafungua mwaka na ngoma hiyo baada ya kutamba na ngoma kadhaa mwaka jana.
Awali wimbo huo ilipagwa kuachiwa mapema kabsaa mwa mwaka huu wa 2014 lakini kutokana na mipango kubadilikia ilibidi zoezi lisimame na kusogea mpaka Tarehe 11.02.2014 ambapo kila kitu kitakuwa kimekwenda kama kilivyopangwa.


0 comments:

Post a Comment