Sunday, December 22, 2013
BAADA YA KUITANDIKA YANGA KOCHA WA SIMBA AMERUDI KWAO
11:34 PM
No comments
Baada ya kuipa timu yake ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga (Nani Mtani Jembe), Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic 'Loga',
aliondoka nchini jana usiku na kwenda kwao Croatia kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya huku akiahidi makubwa zaidi atakaporejea.
Mcroatia huyo atakosa mechi mbili za hatua ya makundi katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yatakayofanyika kuanzia Januari Mosi mwakani.
Logarusic alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu kwake katika dakika 15 za kwanza kwa sababu alihitaji muda wa kuwasoma wapinzani wake na kuimarisha kikosi chake haraka pale alipobaini kuna upungufu.
"Kila mechi ina ushindani wake na mipango yake, kikubwa ni kumsoma mpinzani wako na kujipanga kumkabili, ndivyo nilivyofanya na nilifanikiwa," alisema Logarusic.
Aliongeza kwamba anaondoka lakini ameacha programu ya mazoezi itakayokuwa chini ya kocha msaidizi, Selemani Matola.
0 comments:
Post a Comment