Mwanamuziki
Linex Sunday Mjeda ambaye asili yake ni Kigoma na anafanya poa katika
muziki wa Bongo fleva amefunguka na kusema kuwa kwa mwaka huu
ataanza
kumjengea nyumba Mama yake mzazi ambae anaishi Kigoma.
Linex
ameweka wazi mpango wake huo wa kumjengea mama yake nyumba ambayo
amedai haitakuwa ya Mamilioni ya pesa ila nyumba ambayo mama yake
atakumbuka kuwa Mwanae Linex ndie kamjengea kwa gharama yake kama
zawadi ya kumzaa na kumlea katika mazingira magumu ya shida sanaa.
Mbali
na hilo msanii huyo amekili wazi kuwa hajawahi kumfanyia Mama yake
jambo lolote lile kubwa katika maisha yake na hiyo ni kutokana na
ukweli kwamba alikuwa akitafuta maisha na kupambana na maisha.
“Ujumbe
huu umfikie mama angu sijawahi kukufanyia jambo lolote kubwa katika
maisha cos mwanao nilikua napambana lakin nakuahid mama kitendo cha
kunizaa mwanao siku ya wapendanao /Valentine sikulipi fadhila but
mwaka huu ntastart kukujengea nyumba ambayo si ya mamilion ya pesa
but nyumba ambayo utakua mwanao Sunday kakujenge kukushukuru kwa
kumzaa valentine na kumlea katika mazingira magum ya shida
sanaaaaaaaaa”
0 comments:
Post a Comment