Akizungumzia
mgogoro wa ardhi wa Loliondo Waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utarii mchungaji msingwa amesema kuwa Mgogoro huo
wa Loliondo umejengwa na serikali iliyopo madarakani hivyo serikali
haina nia ya kutatua mgogoro huo.
Msigwa amesema kuwa
tunapozungumza masuala ya masirahi ya taifa ni bora kuachana na siasa
zisizo na maana kwani wote wapo katika boti moja hivyo busara
ichukuliwe na mawazo ya watu wa pande zote wanahusika.
Msigwa
amesema kuwa serikali ya Chama cha mapinduzi inahusika moja kwa moja
na masuala ya ujangiri kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wa viongozi
wanao hujumu mariasili ya taifa letu la Tanzania.
Serikali
inahusika moja kwa moja katika ujangiri na migogoro ya ardhi iliyopo
ndio maana serikali ya chama cha mapinduzi na viongozi wake hawana
kauli yoyote ile juu ya masuala hayo.
0 comments:
Post a Comment