Friday, May 3, 2013

LULU-KIMYA CHANGU KINA MAJIBU MENGI


Msanii maarufu Lulu Michael ambae hivi karibuni alitoka nje kwa dhamana kufuatia kesi inayomkabili ya kuuwa bila kukusudia,amefunguka na kuonesha kukerwa na magazeti pendwa nchini kutokana na kuandamwa kuandikwa kwa skendos zisizo na ukweli ndani yake kwa mujibu wake.

Lulu ametoa angalizo kwa magazeti hayo pendwa baada ya gazeti moja kuandika Habari iliyokuwa na Kichwa cha habari kuwa
Lulu, wema, Diamond afya mgogoro” baada ya gazeti hilo kwenda uraiani na bidada huyo kupata taarifa na kusoma habari hiyo alifunguka katika mitandao ya kijamiii na kuandika hichiii hapa.

..Imekuwa ni kawaida ya mtu kujisikia kusema chochote...muda mwingine mnaweza mkahisi hatuoni au mkahisi kukaa kwetu kimya ni wajinga!!mm kama mm napenda kuwajulisha kuwa LULU mliyekuwa mnamjua sio LULU wa ss...msitegemee kusikia nabisha au kupigizana kelele...fanyeni kazi yenu lakini sio kuchafuana na kuipotosha jamii....!!!nadhani kimya changu kina majibu mengi..



yote kwa yote natoa rai kwa wasanii ambao wanaona hawatendewi haki na kuandikwa vibaya katika magazeti hayo pendwa kuwa wanaweza kuwakilisha malalamiko yako katika vyombo vinavyotambulika kiserikali na kupata staiki zao mfano LULU unaweza kwenda MCT na kuwakilisha malalamiko na yakafanyiwa kazi na kama utakuwa umeonewa kweli wataomba radhi kama si kukulipa.

0 comments:

Post a Comment