Mwanasiasa
na Mayor wa Manispaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ameonesha kuumizwa kwa
kupotea kwa kundi la Muziki wa bongo fleva Chemba Squad lililokuwa
likifanya poa katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva miaka kadhaa ya
nyuma.
Silaa
ameoneshwa kuumizwa na ukimya wa wanamuziki hao kwa sasa ingawa
ameonesha kukumbuka mambo mengi ya nyuma baada ya kuonana na member
mmoja ofisini kwake ambae ni Noorah
“Just
met Nurah in my office, amenikumbusha mbaaali! Chemba squad! Maisha
haya! Sad, simsikii sana”
Kundi
la Chemba Squad liliundwa na wakali kama Gwair Cow Boy,Noorah a.k.a
Babastlyz,Mez B mzee wa Kikuku pamoja na Dark Mastar na kufanya poa
sana kwa ngoma zao kama kundi na ngoma zao kama mtu mmoja mmoja
katika kundi.
Noorah
siku za karibuni alitoa wimbo wake mpya uliokwenda kwa jina la Nikupe
nini alimshirikisha Msanii Ally Kiba 4 real na kufanya poa katika
radio mbalimbali hapa town.
0 comments:
Post a Comment