Tuesday, May 28, 2013

DUDE AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI


Msanii wa Filamu Tanzania Kulwa Kikumba alimarrufu kama Dude amepata na pigo baada ya kupata msiba wa Mama yake mzazi leo jijini Dar es salaam .

Mama mzazi wa Msanii Dude amefariki asubuhi ya Leo majira ya Saa Kumi na mbili,baada ya kupata taarifa juu ya kufariki kwa mama yake Dude alitoa neno lake kwa wadau kwa kusema.

Ndugu zangu wapendwa nimefiwa na Mama mzazi niliempenda kuliko mtu yoyote yule dunia hii”

Hii ni picha ya Dude akiwa na Marehemu Mama yake asubuhi ya leo wakati akimpeleka Hospitali



Mungu akupe nguvu katika wakati mgumu huu kwako Dude.

Sisi tulimpenda lakini mungu kampenda sanaa,apumzike kwa Amani.

0 comments:

Post a Comment