Wednesday, May 29, 2013

MIKASI ULINISUKUMA KUFANYA KAZI NA NGWEA-SILAA



Mayor wa Manispaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ambae jana alikuwa 
amezungumzia juu ya kundi la Chamber Squard lilikuwa limeundwa na Albert Mangwea,Noorah,Mez B pamoja na Dark Master.

Mh Silaa amesema wimbo wa Albert Mangwear wa Mikasi ndio wimbo uliomuhamasisha kufanya kazi na msanii Huyo mwaka 2004 wakati Jeery Silaa alipokuwa Waziri wa Social katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam

Mitungi,blantii,mikasii..wimbo huu ulinifanya nifanye kazi na Ngwea 2004 nikiwa waziri wa social UDSM. Lala kwa amani Ngwea.....”amesema Silaa.

Albert Mangwear amefariki Dunia Jana Nchini South Afrika Johannesburg katika Hospitali ya St Helen Joseph.Msiba upo maeneo ya Mbezi Beach japo Taratibu za mazishi zinaweza kufanyika Morogoro sehemu alipozikwa Baba yake.

0 comments:

Post a Comment