Thursday, May 30, 2013

COW BOY NJOO UONE SIMANZI YA TAIFA JUU YAKO-MRISHO MPOTO



Msanii maarufu wa miondoko ya Kughani Mrisho Mpoto anaefahamika kwa jina la Mjomba Jana alipofika katika Msiba wa Msanii Mwenzake Maeneo ya Mbezi Beach akionekana kushikwa na Uchungu alipoona namna Sauti za Wazee kwa Watoto wakilia kwa uchungu baada ya kumpoteza Kijana wao mpendwa aliefariki siku ya Tarehe 28 huko nchini South Afrika.

hata uwe na roho ngumu kama mpingo, ukifika nyumba hii utalia tu, ukisikia sauti za wazee na watoto zikipokezena kulia kwa uchungu.. unaweza kusema neno likamchukiza mungu!. cow boy njoo uone simanzi hii ya kitaifa juu yako”

Mrisho Mpoto alifika Msibani hapo kuwafariji ndugu jamaa na Marafiki walioguswa moja kwa moja na msiba huo na baada ya kusaini Kitabu cha Wageni na kwenda kuketi ndipo alipotafakari na kuona watu walikuwa na mapenzi na Albert kwani wengi wao walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa kutokana na kifo cha Kijana huyo kuwa ni cha Ghafla.

Mwili wa msanii Albert Mangwear unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumamosi kutoka nchini South Afrika na kuletwa Tanzania kwa maandalizi ya maziko yatakayofanyika Mjini Morogoro.

MRISHO MPOTO AKISAINI KITABU CHA WAGENI JANA MSIBANI MBEZI 

0 comments:

Post a Comment