Msanii
wa Filamu Nchini Tanzania Stanley Msungu jana amenukuliwa akitoa
lawama kwa kamati ya mazishi ya Msanii Ngwear kwa kutofanyia vikao
vyao Msibani.
“kikawaida
kamati za mazishi hufanya vikao vyao msibani sasa kamati ya mzishi ya
ndugu yetu ngwea hatuielewi mnafanyia wapi vikao vyenu? tunaona
taarifa tu kwenye mitandao lakini msibani hatuwaoni mda huu mnafanyia
wapi vikao?”
Kitendo
cha Kamati ya mazishi kutofanyia Vikao hivyo Msibani kumepelekea
Baadhi ya watu kuona hakuna ulazima wa kufika nyumbani moja kwa moja
wakati kuna wafiwa wanahitaji Faraja kutoka kwetu pindi watuonapo
wanafarijika kuona tupo pamoja nao.
Kwa
mujibu wa Stanley majira ya saa Saba Mchana Jana Msibani kulikuwa na
watu wachache sanaa na Wasanii waliofika kwa kipindi ambacho yeye
alikuwepo ni Kara jeremiahar pamoja na Mrisho Mpoto,na akatoa rai kwa
wasanii wenzake kufika Msibani ili kuwafariji wafiwa waliopo katika
wakati mgumu huu.
“kiukweli
watu ni wachache sana, tangu nimefika tena leo saa saba mchna
hatufiki 20 na wasanii waliofika tangu mimi nipo hapa mpaka mda huu
hasa ukinitoa mimi na mdogo wangu noster ni kala jelemiah na mrisho
mpoto najua wenda walikuwepo wakati mimi sipo wameondoka lai yangu
tuje msibani ndugu zangu tuwajibike na kila kinachoendelea”
BWANA
AMETOA BWANA AMETWAA.
0 comments:
Post a Comment