Msanii
Bushoke alietamba miaka ya nyuma na Ngoma zake kibao kama Watashindwa
lala,Dunia Njia na zingine kibao ambapo kwa sasa amehamishia makazi
yake Nchini South Africa,ameonesha kukerwa na baadhi ya waandishi wa
Mitandao ya Kijamii pamoja na na wale waliopo katika vyombo vya
Habari kwa vitendo vya kupotosha jamii na kutokuwa na utu miyoni
mwao.
Msanii
huyo amefunguka hayo jana baada ya kuona na kusoma ripoti iliokua
ikisambazwa katika vyombo vya habari ikieleza chanzo cha kifo cha
Msanii Ngwear,kwa mujibu wa Bushoke amesema kuwa ile ripoti
haikutolewa na madaktari kutoka katika Hospitali aliokuwa amelazwa
marehemu bali ni mtu tu aliunda na kuitawanya ili aweze kupata
wasomaji wengi katika Blog yake au gazeti lake.
Vile
vile Bushoke alioneshwa kukerwa na kitendo cha mtu aliepiga picha
mwili wa marehemu wakati wapo katika chumba cha kuifadhia Maiti akiwa
bado hata ajaandaliwa,amedai kuwa kitendo hicho ni sawa ni kumkosea
marehemu na kuendelea kumfedheesha na kuikosea familia,ndugu na
rafiki wa marehemu.
“kiukweli
nikekerwa sana na Mtu aliepiga picha ya mwili wa marehemu kwani ni
kuendelea kuiumiza familia,Ndugu na Marafiki wa marehemu,sijui lengo
lake lilikuwa nini wakati sisi tulipiga marufuku kupiga picha pale
lakini yeye kapiga picha Mwili wa Marehemu ukiwa hata
haujaandaliwa,hili jambo si ungwana na si haki kabsa,akumbuke Dunia
tunapita tuu.
0 comments:
Post a Comment