MCHEZA sinema na muimbaji wa bongo fleva
anaemiliki kampuni ya Shilole Classic amefunguka na kusema kuwa wasanii wa
filamu wametawaliwa na majungu na kutokuwa na upendo wa kweli kati yao hali
ambayo huwafanya kutokuendelea kwani muda mwingi huutumia kufuatilia maisha ya
watu.
Shilole alifunguka maneno hayo alipokutana katika
one to one interview na Mpita njia katika Hoteli ya Lamadar jijini Dar es
salaam alisema kuwa wasanii wa bongo fleva wamekuwa na upendo kati yao na
wanashirikiana katika mambo mbalimbali hata nje ya kazi zao lakini si kwenye
tasnia ya Filamu.
![]() |
SHILOLE |
Aliendelea kutiririka kuwa katika mwaka wa jana
kutokana na ushirikiano mzuri alioupata kwa wasanii wa bongo fleva umemsaidia
yeye kufanya show nyingi mno kwa wasanii wa kike Tanzania hayo mafanikio
yamekuja kutokana na ushirikiano mzuri alioupata kutoka kwa wasanii wa bongo
fleva.
0 comments:
Post a Comment