Na Kitalima Gerald
WASANII wachanga wa Filamu wameombwa kujitokeza
kwa wingi katika Tamasha la Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) litakalo
fanyika siku ya Jumamosi ya Tarehe 26 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar
Live.
Wito huo ulitolewa na Rais wa Shirikisho la Filamu
Simon Mwakifwamba alipokuwa akieleza lengo la tamasha hilo.”wasanii wachanga
wajitokeze kwa wingi siku ya tamasha kwani ndio sehemu yao kuonesha vipaji vyao
siku hiyo kutakuwa na wasanii mbalimbali hivyo wanaweza pata fursa ya kuonekana
na wakapewa nafasi na wakongwe katika kazi zao”
![]() |
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simoni Mwakifwamba |
Akizungumzia wasanii wa filamu watakao fanya show
katika muziki ni pamoja na Shilole,Sunura,Joti,Masanja Mkandamizaji,Hemedi
‘PHD’,Kitale lakini Twanga pepeta,Tundaman pia watafanya show kali siku ya
Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment