Na Kitalima Gerald
MUIMBAJI na mcheza sinema za bongo Snura Mushi
mtoto wa kibosho anaetamba na kibao cha majanga amefunguka na kusema hakuna
star bila shabiki.
Snura amefunguka hayo pale alipokuwa akiwaomba
watanzania wajitokeze kwa wingi katika tamasha lililoandaliwa na Shirikisho la
Filamu Tanzania (TAFF)litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live siku ya
Jumamosi ya tarehe 26
“Nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi waje
kupata raha na kubadilishana mawazo na wasanii mbali mbali nikiwemo mama yao
Snura,Shilole,Joti,Hemedi,Masanja mkandamizaji,Twanga pepeta maana hakuna
super star bila shabiki hivyo watokeze kwa wingi kutuenzi na kutufaliji”
![]() | |
SNURA MUSHI |
Onesho hilo limeandaliwa na Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF) likiwa na lengo la kukutanisha wadau mbalimbali ambao
watalisaidia shirikisho la filamu Tanzania kuweza kupata vifaa vya ofisi na
kupata ofisi inayoendana na hadhi ya shirikisho.
0 comments:
Post a Comment