Na Kitalima Gerald
MKALI wa bongo flava Richard Mavoko anaetamba na
ngoma kama mary me,silali na One time amefunguka na kusema asingeweza kufanya
vizuri katika muziki wa bongo fleva angekuwa mchezaji wa msimbazi.
![]() |
Mavoko aliendelea kutiririsha ukweli huo kwamba
kabla ya kufanya muziki alikuwa mchezaji mzuri wa soka na alikuwa akichezea
namba 9 na katika soka alifahamika kwa jina la ‘Etoo’ kutokana na uwezo wake wa
kufumania nyavu za wapinzani wake kila alipocheza mechi.
“Kweli kabsa walikuwa wakiniitaEtoo kwani ukicheza
na mimi ni lazima nikufunge utake usitake haijawahi kutokea nicheze mechi
halafu nisishinde,nilishaanza kufanyiwa mpango wa kwenda kucheza soka Simba
FC hivyo kipaji cha soka kipo na kama
muziki ungenishinda ningesakata
kabumbu na watanzania wangenielewa tu”
Pindi alipoulizwa ni kwanini angecheza Simba na si
Yanga alidai kuwa yeye ni mnazi wa Msimbazi
hivyo angecheza Simba kwakuwa na
mapenzi na Club hiyo na ndoto ya kucheza soka ilikufa pale alipoweza kufanya
vizuri katika muziki wa bongo flava.
![]() | |
RICHARD MAVOKO |
Akizungumzia
ngoma yake mpya One Time ambayo amefanya chini ya C9 amesema wimbo huo
amemzungumzia mwanaume ambae anampango wa kuongea na msichana asie na wazo na huyo
mwanaume,”video ya one time inafanywa na Adam Juma wa Visual Lab hivyo muda si
mrefu itakuwa tayari luningani”Mavoko alisema.
0 comments:
Post a Comment