Tuesday, April 1, 2014

MANGWEA KANIACHIA ZAWADI-BLACK RHINO

MSANII nyota wa Bongo fleva ambae ni mdogo wa msanii Prof Jay, Black Rhino ameweka wazi kuwa kabla ya kifo cha mwanamuziki Albert Mangwea alifanya nae
kazi chini ya produza Mbezi,kazi hiyo aliyoipa jina la Lookie lookie my life ambayo yeye anaiona ni kama zawadi aliyoachiwa na marehemu Ngwea kutokana na mazingira ya kazi hiyo ilivyofanyika.

Black Rhino alisema haya alipokuwa akizungumza katika kipindi cha E news kinachorushwa kupitia televisheni ya vijana EATV.

"Lookie Lookie my life ni wimbo wangu wa kwanza kwa mwaka huu 2014 kuachia nimefanya na marehemu Ngwea chini ya pruduza Mbezi kiukweli ukiangalia mazingira ya ufanyaji kazi katika wimbo huu naweza kusema Ngwea ameniachia wimbo huu kama zawadi baada ya kifo chake,hivyo katika wimbo huu tumezungumzia watu ambao wana angalia maisha ya mtu badala ya kuangalia maisha yao binafsi hivyo tunawataka watu hawa kuangalia maisha yao na si maisha ya mtu ili mambo yaweze kwenda mbele na kufanya maendeleo yao binafsi."

Black Rhino hajaweka wazi ni lini haswa wimbo wake mpya utatoka baada ya kimya chake cha muda mrefu katika muziki ingawa amedai kuwa itakuwa ni kabla ya mwezi wa nne,mkali huyu alishatamba na ngoma kama Black Chata,Mistari,Usipime na zingine.

0 comments:

Post a Comment