MSANII
wa muziki wa kizazi kipya Hamisi Ramadhani Baba,maarufu kama
'H.Baba' amefunguka na kusema kuwa wanamuziki wa Bongo fleva sasa
watakata
mauno,H Baba alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwa njia ya
simu na Gazeti hili jana.
H
Baba amesema kuwa wakati anatambulisha muziki wa Bongo Bolingo Fleva
wadau wa mauziki kama hawakuweza kumuelewa na hawakuweza kumpa
support ili muziki huo ufike sehemu nzuri zaidi lakini anashukuru
sasa aina ya muziki aliokuwa akiupigania miaka kadhaa nyuma ndio
umeliteka soko la muziki wa Afrika na unazidi kukua kwa kasi kubwa.
"Wakati
nimeanza kufanya Bongo Bolingo Fleva watu hawakunielewa nafanya nini
na kuna baadhi ya wasanii wenzangu walikuwa wakinikashifu kuwa H Baba
yule ni mkata viuno tu,sasa kwa kuwa muziki huu ndio umeshika chat
kwa sasa amini usiamini wasaniii wa Bongo Fleva sasa watakata viuno
kama H Baba maana muziki huu unahitaji uwezo wa hali ya juu katika
steji ndio maana hata watu ambao wanaufanya wapo vizuri stejini".
H
Baba aliongeza kuwa kwa sasa wasanii wakubwa Africa kama P square,Iyanya,Davido na wengine wengi wanafanya muzuki ambao yeye
anafanya hivyo kwa kuwa wasanii wengi wamekuwa si wabunifu kubuni
vitu vyao hivyo wataanza kufanya huo muziki ila wanapaswa tu kuelewa
kuwa muziki huo unahitaji uwezo mkubwa stejini.
Mimi
nashukuru sana P Square kuweza kutoa wimbo wao huu wa Test my money
ambao umekuwa na vionjo vya bolingo kama ambavyo mimi nafanya Bongo
Bolingo fleva maana wimbo huu utasidia aina ya muziki huu kukua na
kuenea zaidi na hii itanisaidia mimi maana wao watakuwa wamefanya
kazi rahisi kuwaelewesha wadau juu ya aina hii ya muziki ninao fanya
hivyo inaweza kunipa nafasi kufanya mambo mazuri zaidi,hivyo hawa
wasanii wa Bongo fleva najua watafanya huu muziki lakini wanapaswa
kutambua kuwa uhahitaji uwezo wa hali ya juu ukiwa stejini,hivyo
wajipange kukata mauno tu.
Akizungumzia
Wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tubebane,H Baba amedai kuwa
wimbo huo hakuutambulisha bali umevuja baada ya gari yake ndogo
kuvunjwa kioo na kuibwa kwa baadhi ya vitu ikiwemo Flash ambayo
ilikuwa na wimbo huo ndipo ilivuja,amedia kuwa haukuwa wakati wake
kuachia wimbo huo kwa sasa kwa kuwa bado alikuwa akiendelea kujiandaa
ili kuja kutambulisha wimbo huo siku za usoni.







0 comments:
Post a Comment