Tuesday, April 1, 2014

CHRISTIAN BELLA AIGEUKIA BONGO FLEVA

MWANAMUZIKI na Mmiliki wa Bendi ya “Malaika music band” Christian Bella ameamua kujitupa kufanya muzuki ambao utakuwa tofauti kidogo na iana ya
muziki ambao amekuwa akifanya kwa miaka kadhaa,akiwa na lengo la kuleta ladha tofauti katika muziki wake na kujiongezea mashabiki ambao anawakosa kwa kufanya muziki wa band tu.

Christian Bella alisema kuwa kwa sasa anaanza kutambulisha wimbo wake mpya ambao amemshirikisha msanii Ommy Dimpoz,wimbo ambao umefanywa katika studio za Combination Sound chini ya produza Man Walter.

Ni kweli nimefanya aina tofauti ya muziki kwa sasa natambulisha Bongo fleva niliyofanya na rafiki yangu Ommy Dimpoz,wimbo unaitwa 'Nani kama mama' na nitautambulisha mwezi April mwanzoni,nitatoa Audio na Video kwa pamoja ili mashabiki waweze kupata burudani na kupata kumsikia na kumuona Bella akifanya Bongo Fleva"

Christian Bella aliongeza kuwa huo ni mpango wake kwa sasa kuchanganya ladha katika muziki wake hivyo mashabiki wakae teyari tu kwani kuna wimbo wa RNB utafuata baada ya Nani kama mama,wimbo ambao anafikiri kufanya na mwanamuziki wa Rnb wa hapa nyumbani huku akichanganya na msanii mwingine wa Hip Hop.

Christian Bella alishawahi kuwa Prezidaa wa Bendi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masauti' kwa miaka kadhaa kabla ya kuachana na Bendi hiyo na kuanzisha Bendi nyingine inayofahamika kama 'Malaika music band”.


0 comments:

Post a Comment