MSANII
wa muziki wa Bongo fleva ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya
'Tuongeze bidii' amesema kuwa vijana wa kitanzania wajitaidi kubadili
mtazamo wao na kukiangalia kilimo kama mkombozi ,kuliko kuendelea
kung'ang'ana na vitu ambavyo haviwezi kubadili maisha yao, licha ya
kufanya muziki Ditto ameamua kuwekeza katika kilimo na kutegemea
kilimo kubadili maisha yake kama kijana.
Ditto
alisema kwa sasa anafanya muziki na amewekeza katika kilimo cha ufuta
na nanasi kilimo ambacho ni cha kisasa na anategemea kunufaika na
kilimo hicho kwani kabla hata ya kuanza kulima alishafanya uchunguzi
wa kutosha na kugundua kuwa inawezekana ndipo alipo amua kufanya
kweli.
"Ninafanya
kilimo cha ufuta na nanasi ninamiliki zaidi ya ekali kumi
Bagamoyo,lakini kilimo nachofanya ni kilimo cha kisasa kwani kuna
vijana ambao wanasimamia na kufanya kazi na mimi nakuwa nafuatilia
nini kinaendelea na kitu gani kinahitajika na kutimiza,vijana
wanapaswa kufunguka na kubadili mawazo yao maana kilimo ni njia
mbadala ya kujiongezea kipato na kubadili maisha yao,lakini siwezi
kuwalaumu vijana maana huenda wanakosa taarifa sahihi na pia wanakosa
ubunifu ndio maana wanashindwa kuziona fursa kama hizi."
Mbali
na hilo msanii Lameck Ditto amewalaumu watu ambao wamefanikiwa katika
maisha na hawataki kuwa mwongozo kuwashauri au kutoa siri ya
mafanikio yao kwa jamii na kufananisha kitendo hicho ni sawa na
ubinafsi wa kutaka maendeleo peke yako.
Wakati
mwingine siwezi kuwalaumu moja kwa moja vijana kwani hata watu ambao
wanafanikiwa kimaisha unapowauliza juu ya mafanikio yao wanabaki tu
kukuambia komaa,wamekuwa ni wachoyo wa mawazo na wabinafsi wenye
kutaka maendeleo ya kwao peke yao,ndio maana vijana wengi wanakosa
taarifa muhimu ambazo zingiweze kuwasidia kufanya jambo fulani kwa
maendeleo yao."
Lameck
Ditto ametoa wito kwa vijana kuacha masuala ya kuigana katika
biashara,sanaa au katika jambo lolote lile bali wajifunze kutafuta
taarifa ambazo zitasaidia kuwa chachu katika maendeleo na kutokuogapa
kufanya jambo wasichoke kujaribu na kujituma zaidi maana ndio siri
kubwa ya mafanikio kwa binadamu.







0 comments:
Post a Comment