Tuesday, April 1, 2014

JAY MOE,NATURE ,PROF JAY WAIFAGILIA JWTZ

WAKONGWE wa muzuki katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva Jay Moe,Juma Nature pamoja na Prof Jay wametunga wimbo kutoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika kulinda nchi na kutatua matatizo mbalimbali nchini,wimbo huo unatarajiwa kuachiwa rasmi mwezi wa nne Audio pamoja na Video.

Akizungumza Mtayarishaji wa video ya wimbo huo Mike Tee alisema kuwa Video ya wimbo huo ilishakamilika muda mrefu toka mwaka jana na ilipagwa kuachiwa toka November mwaka jana lakini kuna mambo yalikuwa hayajakamilika kiutawala kitu ambacho kimefanya mpka leo kazi hiyo iwe bado haijatoka.


"Wimbo ulikuwa utoke toka mwaka jana November ila aliyekuwa akisimamia ili kazi ikamilike ametengeneza ukuta kati yangu mimi na wakuu wa jeshi, ndio maana nimeamua kutoa wimbo huo mwezi ujao kama zawadi,ila version yangu tofauti na kazi niliyokuwa nikifanya awali pamoja na jeshi."

Mike Tee alidai katika ufanyaji wa Video hiyo kulikuwa na changamoto kubwa sana hususani katika kupata vibali kwani kulikuwa na usumbufu sana,pia kuna sehemu ambazo hawakupewa ruksa kabisaa kushoot scene za video hiyo lakini pia kazi walikuwa wakifanya kwa amri.

"Kwanza ilikuwa usumbufu wa kupata vibali,kuna sehemu unaweza ukashoot ukaambiwa hauruhusiwi ,pia upande wa malipo wamekuwa wasumbufu kifupi kazi imeisha toka mwaka jana lakini nasumbuliwa sana,upande mwingine wanafanya kazi kwa amri hawajui muda mzuri wa upigaji picha hivyo imekuwa shida kidogo wakati wa ufanyaji kazi katika video hii."

Katika wimbo huo unaokwenda kwa jina la (JWTZ) uliowakutanisha wakongwe wa muziki Tanzania umefanywa katika Studio ya Bongo Record chini ya P Funk majani,huku Video ya wimbo huo ikiwa imefanywa na Director Mike Tee Mnyalu.

0 comments:

Post a Comment