Wednesday, February 19, 2014

UNAFAHAMU KUWA KUNA BAADHI YA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA LEO WAMEOMBA KUONGEZWA POSHO ETI LAKI TATU NI NDOGO?SOMA HAPA.

NCHI HII ITAMALIZWA;
Julius S. Mtatiro


Tunafahamu kuwa kuna njama zinapangwa ili wajumbe wa bunge la katiba ati waongezewe fedha zaidi.Hoja hii imetolewa leo hii na mmoja wa wajumbe huku ikionekana kuwa maarufu na inayoungwa mkono na baadhi ya wajumbe, hasa wabunge wa CCM.

Binafsi na wenzangu wengi tumepanga kutumia kila uwezo kuzuia nia hiyo OVU, ifikie wakati tuambiane ukweli vinginevyo nchi hii watu watakufa masikini.

Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku zinatosha kabisa, ambaye hazimtoshi aongeze za kwake, na ambaye anaona hawezi kuongeza zake aondoke Dodoma ili kupisha wanaoweza kutunga katiba kwa posho ya shs 300,000 waendelee.

Laki tatu tunazopata zinatosha kila kitu na CHENJI inabaki, zinatosha kula, kulala, kumpa dereva na kuishi Dodoma.

Lazima sisi tunaotunga katiba tufahamu kuwa maisha ya wananchi ni muhimu na kwamba wana mahitaji yasiyokwisha hata baada ya bunge hili.

Baadhi yetu tulioko humu bungeni tutakataa jambo hili kwa maneno na vitendo. Wakipitisha kwa wingi wao tuta-boycott kuzipokea.

Kenya pale mnakumbuka hoja ya wabunge kujiongezea mapesa ilipingwa vikali na wananchi waliandamana hadi nje ya ukumbi wa bunge. Hapa Tanzania hata zikiongezwa milioni kila siku hutaona mwananchi anachukua hatua kwa vitendo, kuoneshwa kutoridhishwa kwake.

Tuna tatizo kubwa sana, sisi viongozi na wananchi wetu. Kuna mtu anasema, viongozi ni zao la jamii hiyohiyo.

Tuungane pamoja kusimamia jambo hili, ninyi mlioko nje na sisi tulioko ndani.




0 comments:

Post a Comment