NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo ni siku ya Bahati kwako utapata fedha au utapata faida ambayo
hukuitegemea au utasamehewa makosa ambayo uliyomfanyia mtu wako wa
karibu awe mumeo, mkeo mpenzi wako au mshirika wako.
SAMAKI –
PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku hii ya leo kuna mgeni na kitu
kilichopotea ambacho unataka sana kujua habari zake.inaonekana
unawaza juu ya nafsi yako,unataka kujua maisha na hali yako
itakuwaje. Pana kazi au jambo ambalo unashaka nalo kama litatimia au
vipi? Elewa kwamba utapata furaha kazini kwako au utaletewa biashara
ambayo itakuletea faida kimaisha
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR
20)
Leo inaonekana una hamu sana ya kukutana na mpenzi wako na
kujua juu ya safari au biashara na kazi. mambo yako yataenda vizuri,
Unashauriwa kuwa uwe mtulivu na hali yoyote itakayokutokea siku ya
leo kwa kuwa ni hali ya muda mfupi tu.
NG’OMBE – TAURUS
(APR21 – MAY 20)
Leo Haja yako itatimia. Kuna mtu mkubwa mmoja
ndiye atakaye kuonea huruma kwa njia usiyoitegemea. mgonjwa wako
aliye hospitali atapona au utaletewa habari ya nzuri
itakayokufurahisha..
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Unashauriwa kuwa makini na kila unachotaka kukifanya, usimamizi
wa karibu unahitajika kwa kila jambo unalotaka kulifanya. Mambo yote
unayotaka utayapata kwa sharti uache kuwa na wasiwasi na hofu au
kupapatika, mambo yako mengi yatakwenda kwa kusuasua,
KAA -
CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo lazima utapata kitu unachokitaka au
pesa unazohitaji au mtu unayemtarajia. Mtoto au kitu kilichopotea
kitarejea mambo yako mengi yatasimama, yale tu utakayoyafanya wewe
mwenyewe ndiyo yatakayofanikiwa, lakini yale yote utakayoyaagiza
yafanywe na watu wengine yatalala.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG
22)
Jumatano ya leo ni Njema sana kwako Lazima utapata kitu
unachokitaka au pesa unazohitaji au mtu unayemtarajia. Pamoja na hayo
jaribu kuwa na tahadhari unaweza kupatwa na balaa la bila ya
kutegemea na bila kosa lolote na hata kama lipo kosa basi kosa hilo
hukulifanya wewe.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo ni
siku ambayo
,itakubidi utoe rai nzuri na uache woga na usivunjike
moyo kwani patatokea upinzani na undani, kuna habari za uongo
utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana na biashara zako. Jaribu
kufanya uchunguzi kabla hujachukua hatua.
MIZANI - LIBRA (SEPT
24- OCT 23)
Safari unayofikiria ni nzuri, na biashara yako
itafanikiwa maendeleo yako yatakuwa ni madogo na yatakuwa yanaenda
polepole sana. Biashara yako pia itapanuka kwa kusuasua.
NGE -
SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo ni siku nzuri kwako Mpenzi wako
atarejea salama, na utashinda mitihani na adui yako atajuta Hii ni
wiki nzuri ya kurekebisha makosa yote ambayo umeyafanya katika
kipindi cha nyuma.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Leo
Unashauriwa kuwa kufanikiwa kwa mambo yako kunahitaji wewe uanze
kujishughulisha na mambo hayo mara moja wala usisite site.Jambo baya
kwako ni kuwa kama kuna mgonjwa hapo nyumbani kwako, lakini kama kuna
mjamzito basi atazaliwa mtoto wa kike
MBUZI - CAPRICORN (DES
22 – JAN 20)
Mambo yote unayoyataka yatatimia kati ya leo na
Jumatano au Jumamosi ijayo usiku. Pengine katika mwezi wa
machi,Tegemea kujionea mambo mengi ambayo ulikuwa umefichwa kwa muda
mrefu na watu wako wa karibu. Ili kuleta baraka leo nenda
kawatembelee wazee wako.
0 comments:
Post a Comment