Mkali
Ney wa mitego anaetamba na ngoma yake ya Nakula ujana amefunguka na
kuweka wazi kuwa kazi zake kwa sasa hawezi kufanya na
wasanii ambao
ni longolongo bali atafanya kazi na wasanii ambao wanatambua nini
wanafanya katika muziki.
Ney
amebainisha hayo alipokuwa akiweka wazi mikakati yake kwa mwaka huu
2014 ambapo amekili kuhitaji kufanya kazi na msanii Joseph Chameleone
wa Uganda ambae kwa sasa amedai yupo katika hatua za mwisho za
mazungumzo nae.
Mkali
huyo alizidi kuweka wazi kuwa mbali na kazi hiyo anayotegemea kufanya
na mkali wa uganda,anategemea kuachia wimbo mpya utakufuata baada ya
nakula ujana ambayo ameshirikiana na Diamond Platnum kama ilivyokuwa
katika wimbo wao wa awali muziki gani.
Ney
amesema kuwa Project yake na Diamond Platnum haijaishia katika Muziki
gani tu bali kuna kazi inafuata ameshirikiana nae.







0 comments:
Post a Comment