Thursday, February 20, 2014

NYOTA YAKO LEO IJUMAA TAREHE 21/2/2013

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo ni siku nzuri kwako na kuna dalili nzuri kwa mambo yako kufanikiwa hasa ikiwa wewe ni mtu ambaye una shuguli nyingi za kifedha au
kibiashara, pamoja na kwamba mambo yako yatakuwa yanasinzia au kwenda polepole kinyume na ulivyotegemea usiwe na khofu mafanikio yapo.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Ijumaa ya leo ni siku njema sana kwako nyota zinaonyesha kwamba utashirikishwa katika mazungumzo ya kibiashara ambayo yatakupeleka sehemu nzuri na za kukufurahisha. Tegemea kupata faida katika mambo yako

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo ni siku ambayo unatakiwa uwe na tahadhari sana kwa sababu Kuna dalili ya wewe kutapata matatizo katika shughuli zako kwa kusumbuliwa na watu mbalimbali watakaokujia kutaka msaada au maongezi yasiyo ya kikazi. Vile vile Kuna habari ya kuvunjika kwa safari yako ya mbali.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Huenda kukatokea majibizano kati yako na watu wengi, majibizano ambayo yatakuletea matatizo makubwa usipokuwa makini. Unashauriwa kutulia nyumbani kwako kuliko kutembeatembea mitaani.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Nyota zinaonyesha kwamba Mambo yako yatakuwa na msongamano na matatizo mkubwa, unatakiwa kuwa makini sana katika kipindi hiki cha mpito, na tumia busara au jaribu kupata ushauri kwani kosa dogo tu linaweza kukuleta matatizo.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Kuna siri nyingi ambazo ulikuwa unafichwa na watu wako wa karibu, lakini kati ya leo ijumaa mpaka jumapili utazigundua.. Unaonywa kutokufanya makosa na uyaepuke maudhi, hasa kwa mpenzi wako.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku tau hizi kuna dalili ya kupata maendeleo katika shughuli zako za kibashara na kikazi, lakini kuwa makini sana mambo ya mapenzi kwani kosa dogo tu linaweza kusababisha mfarakano mkubwa kati yako na umpendae.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Hii ni wikiendi nzuri sana kwako Tegemea kupata mialiko katika shughuli nyingi, hali hiyo itakakusababishia mambo yako mengi kusimama, pamoja ha mialiko hiyo unashauriwa kwenda kwenye shughuli muhimu tu.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako ya kibiashara yatakunyookea sana katika kipindi hiki cha siku tatu kuanzia leo ijumaa mpaka jumapili, lakini mambo ya kimapenzi yatakuwa ya kusuasua sana na kunaweza kutokea migogoro ya mara kwa mara.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Hii ni Wikiendi ambayo Maisha yako yatakuwa na furaha sana wewe na mpenzi wako au mkeo au mumeo. Mambo yako kikazi yatakunyookea sana na upo uwezekano wa kupata kila ukitakacho.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Hii siyo wikiendi njema, Unatakiwa kutojihusisha na shughuli yeyote ile inayohusiana na pesa kwani kufanya hivyo ni kujitafutia hasara ya bure.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kati ya leo na Jumapili jaribu sana uwe na tahadhari kwa sababu Kuna dalili ya kupata bahati mbaya kwa Mpenzi wako ambaye nyota zinaonyesha atakuletea ugomvi unaotokana na Wivu. Tumia Busara katika kutatua mambo yako na wala usitumie nguvu, utakwama


0 comments:

Post a Comment