Thursday, February 20, 2014

KAULI YA ZITTO KABWE NA MWANA FA BAADA YA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUKATAA POSHO YA LAKI TATU.

Wajumbe wa Bunge la katiba wamekataa posho ya Laki tatu ambayo ndio ilikuwa imepangwa walipwe kila siku kwa muda wa siku 70 ambazo watakuwepo Mjini
Dodoma kujadili juu ya Katiba,wajumbe hao baadhi wameonesha kutokubaliana na posho iliyokuwa imepangwa awali na kuhitaji kulipwa pesa zaidi kwa siku kwa madai kuwa posho hiyo haitoshi kuendesha maisha ya kila siku mjini Dodoma.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ametoa msimamo wake juu ya sakata hilo na kusema kuwa yeye hawezi kupokea nyongeza ya posho hizokwani kwa kufanya hivyo nae atakuwa katika kundi la walafi ambo yeye amewaona hawana maana.

Naomba niseme wazi kabisa kwamba, sitapokea nyongeza yeyote ya posho hata ikiongezwa. Inaweza isisaidie kuzuia walafi wengine kupata posho kubwa lakini ni bora kuhesabika kwamba nimesema hapana. Ifikie wakati tuseme hapana kwa excesses zisizo na maana.

Ninamwomba Rais asikubali kuongeza posho kama baadhi ya wajumbe wa BM wanavyotaka. Wanachopata kinawatosha sana. Nawasihi wananchi mumwombe na ikibidi kumshinikiza Rais kukataa.”

Nae msanii maarufu wa miondoko ya Hip Hop nchini Mwana FA nae amefunguka na kuonesha wazi kuwa hajapenda kitendo cha baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba kudai Posho zaidi ya laki tatu.

Wabunge,laki 3 yenyewe roho zinatuuma hatujajua tu tuwafanyeje kuzuia na mnaiona ndogo..nyie watu,kuweni serious aisee.Kama wanaona haitoshi na wanamaanisha wajiuzulu hizo nafasi zao tujue wana msimamo...tutawakubali sana..


0 comments:

Post a Comment