Monday, February 10, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE TAREHE 11/2/2014

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Wiki hii utapata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha, Kuhusu safari uliyopanga kwenda ina shida kidogo lakini
usiogope.Pamoja na matatizo nenda hiyo safari.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Wiki hii utapata fedha au utapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa madhambi uliyomfanyia rafiki yako. Kuhama hama ni bora kuliko safari ndefu unayotarajia kwenda.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Utapatwa na mambo ya ajabu ajabu, usijaribu kuvuka mto usioujua kina chake kwani upo uwezekano wa kuondoka na maji. Tegemea kupata safari ya ardhini itakayokupeleka sehemu ambayo hujawahi kufika.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Wiki hii biashara ni nzuri, ndoa itatimia ijapo yule anaehusika na mashauri hayupo. kuna ishara nzur kazini au matembezini na upo uwezekano wa kupata bahati huko uendako.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mambo yako yatatimia katika Jumatano, au mwezi wa nane . Ni siku nzuri kwa kila jambo utakalolitenda. Unashauriwa kuanzisha mambo mapya leo kwani ndiyo siku yako nzuri.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Unashauriwa kuwa uwe makini na marafiki wapya watakaokujia siku za karibuni.Hakikisha unafanya sala kwa dini yako au Fanya sherehe au pika chakula watu wale. Kufanya hivyo kutakusaidia kuondokana na matatizo mbali mbali.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Wiki hii ni ya matatizo kwako usiogope taabu kwani lazima taabu itakufikia kwanza ndio uone mafanikio baadae. jaribu kuwa karibu na watu wa dini yako ili kubarikiwa na ikusaidie kuondokana na matatizo yanayokukabili.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Wiki hii kuna dalili ya kuibiwa mali yako au kupoteza vitu vya thamani kubwa, vilevile kuna ishara ya kukimbiwa na Mkeo au Mpenzi wako au Watoto wako. Usiogope maadui hata kidogo.Kuna Mkuu utakutana nae karibuni, shirikiane nae, atakusaidia sana na utapata mafanikio,

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Kuna mambo mabaya yanakujia katika biashara au kazi yako, Mipango yako yote kuhusu biashara ifanya upesi itafuzu. Jihadhari na vikundi visivyofaa hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili wakusaidie.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako yamo hatarini kuharibiwa na wakubwa wa serikali au kidini, Itakubidi ukutane na watu hao na kufanya mazungumzo nao, jaribu sana kupunguza hasira na unatakiwa kuwa mpole kwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Unashauriwa kutosafiria kwa muda huu ili kujikinga na mabalaa. Mgeni atakaporejea ndio mambo yako mengi yatatengemaa. Jaribu kuwa muangalifu na yoyote utakayeshirikiana naye.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20
Adui yako anayekusumbua lazima atapatwa na matatizo makubwa ya Kiserikali au ugonjwa. unashauriwa kuutumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umeyapanga kuyafanya.

0 comments:

Post a Comment