Mwanamuziki
Hisia ambae alikuwa akiwakirisha Tanzania na mshindi wa nne katika
mashindano la Tusker Project Fame kwa mwaka 2013 anatambulisha
ngoma
yake mpya Valentine hii.
Hisia
amefunguka na kusema kuwa wimbo wake huo wa Mawazo ameufanyia nchini
Kenya ambako ndipo muda mwingi amekuwa akifanya shughuli zake za
muziki.
“Valentine's
Day,natambulisha ngoma yetu ya pili iitwayo Mawazo...coming straight
to you kwa mara ya kwanza kabisa... #Hisia #teamhisia #teamtanzania
#upcomingsingle #mawazo #hisia #goodmusic”
Hisia
anatambulisha wimbo wa pili baada ya ngoma yake ya kwanza Just for
you (kwa ajili yako) kufanya poa kwa wakati wake na kuweza
kumtambulisha katika soko la muziki wa afrika mashariki.
0 comments:
Post a Comment