Wasanii
kutoka pande za Morogoro ambao walikuwa chini ya King Afande Selle
watafanya show siku ya Valentine day katika viwanja vya Rock Garden
morogoro
mjini.
Afande
sele amesema kuwa watakutana wanamuziki wa Morogoro na baadhi ya
wasanii kutoka nje ya Morogogoro na kufanya show hiyo kwa lengo la
kutoa burudani kwa Mashabiki wao.
Afande
aliongeza kuwa atatumia fursa hiyo kutambulisha wimbo mpya unaokwenda
kwa jina la MSHENGA kama zawadi ya pekee na elimu kwa wapendanao
wenye mipango mikubwa na malengo ya kuishi pamoja.
“Ni
kweli tutakuwa na Show BAAB KUBWA' kutoka kwa wasanii wakali wa ndani
na nje ya moro nikiwemo mimi mwenyewe Afande Sele The King na timu
nzima ya Watu Pori&Gheto Boyz,bila kusahau disko'taamu'toka kwa
maDj wa nguvu kuanzia saa kumi jioni mpaka usiku mnene.”
Karibuni
saana'wanandugu'kushuhudia nyimbo kibao za sasa na zamani bila
kusahau siku hiyo tutambulisha wimbo mpya uitwao'Mshenga'kama zawadi
ya kipekee na elimu kubwa kwa Wapendanao kwa dhati na wenye malengo
ya kuishi pamoja milele/daima,,,
0 comments:
Post a Comment