Monday, February 10, 2014

MTAM UNIQUE MSANII MWENYE NDOTO ZA DIAMOND PLATNUM

Msanii kutoka Rujewa Mbeya ambaye ameanza game kwa kutambulisha wimbo wake unaokwenda kwa jina la You make me busy ulioufanya kwa kumpa shavu
Ungerground mwenzake Mariot anampango wa kufika level za Diamond Platnum.
Mtam Unique ambae anakili wazi kuwa amekuwa Inspired sana kufanya muziki kutokana na uwezo wa Diamond hususani katika mashairi pamoja na namna ambavyo mkali huyo amekuwa akimiliki jukwaa,amekili kuwa anatamani sana siku moja afike Level hizo.
Alipokuwa akiweka wazi juu ya mipango yake kuhakisha anakuwa katika game na kufanya vizuri amesema anatambua anapaswa kufanya kazi nzuri ambayo itapendwa na watu na kujituma katika kazi ili aweze kutimiza ndoto zake hizo.
Mtam amefunguka na kuweka wazi kuwa anatambua Diamond ameweza kufanikiwa kutokana na uwezo wake na jitihada yake katika kazi pamoja na uvumilivu wake uliomfanya kujifunza vitu vingi ambavyo ndivyo vimekuwa mchango mkubwa kwa maendeleo aliyonayo sasa hivyo,ameahidi kupita njia hizo kama mafunzo kwake ili nae aweze kufikia malengo yake kwa njia yake mwenyewe.
Sikiliza na Download Wimbo huo Hapa




0 comments:

Post a Comment