Msanii
Lady Jaydee ambae amefanikiwa kwa mwaka jana na kufanya vizuri katika
muziki wa bongo fleva kupitia nyimbo zake Joto hasira na Yahaya.
Mwanadada
huyo aliejipatia jina la Annaconda ameanza mwaka kwa kutambulisha
ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Historia ambayo amepanga
kuzindua video ya wimbo huo Jumamosi ya tarehe 8.
kufuata
uzinduzi huo mwanadada Jide ametoa nafasi ya watu 20 kutoka kwa
wapenzi wake kupitia ukurasa wake wa Facebook.
“Video
ya Historia iko tayari na itatoka Jumamosi ya tar 8 february 2014
kwenye party maalum ya kuitambulisha, na kutoka humu facebook
nitaalika watu 20 wa kuja kuiangalia kwa mara ya kwanza kabla
haijaruka kwenye TV zote.. Swali litakuja na 20 wa mwanzo
watakaopatia nitajumuika nao. Usicheze mbali”
0 comments:
Post a Comment