Mshambuliaji
wa klabu ya Yanga Jeryson Tegeta hivi karibuni ameamua kumrudia
mwenyezi Mungu kwa kuzaliwa upya (kuokoka) baada ya kupata ushuhuda
wa
miujiza uliyomkuta mama yake mzazi ambae alikuwa akiumwa na kupata
nafuu baada ya Mchungaji Kumuombea.
Tegeta
siku za karibuni alikwenda nyumbani kwao Mwanza kwenda kumjulia hali
Mama yake mzazi ambae alikuwa anaumwa sana ila kutokana na kupata
maombezi aliweza kupata nafuu na hali hiyo ilimsukuma mshambuliaji
huyo na yeye kuamua kuokoka baada ya kushuhudia miujiza hiyo kwa mama
yake Mzazi.
“Niko
mwanza nimekuja kumuona mama yangu anaumwa sana bt kaja mchungaji
kamuombea mama kapata nafuu kabisa mungu nimkubwa sana na maisha
ukimkabidhi mungu kila kitu kinawezekana maisha ya kidunia hayana
maana bila yesu nimeokoka rasmi get wel soon mama”
0 comments:
Post a Comment