Msanii
wa filamu Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu
anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake,
Steven
Kanumba (28), anatarajia kupanda kizimbani Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam Februari 17, mwaka huu kujibu mashtaka yake kwa mara
ya kwanza.
kesi
ya Lulu itasikilizwa mbele ya Jaji Rose Teemba na mshtakiwa atajibu
mashitaka yake kama ni kweli au siyo kweli.
Mapema
Januari 29, mwaka jana, Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo
kubadilishwa hati ya mashtaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda
mauaji ya bila kukusudia.
Jaji
Mruke alisema kosa linalomkabili mshakiwa lina dhamana kisheria na
kwamba mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kufuata masharti ya kuwa
na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali watakaosaini hati
ya dhamana ya Sh. milioni 20 kila mmoja.
"Tukubaliane
wote kwamba hakuna ubishi roho ya mtu imepotea hivyo sheria lazima
ifuatwe... pia mshtakiwa awasilishe hati zake za kusafiria, kuripoti
kila tarehe Mosi ya mwezi kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam na asitoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha
msajili huyo," alisema Jaji Mruke.
Katika
kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka juzi Vatican,
Sinza jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba bila kukusudia.
0 comments:
Post a Comment