Msanii
Kallah Jeremiah ambae ameweza kufanya vizuri kwa mwaka jana na ngoma
zake mbali mbali ambazo zimefungua njia na kumuongezea heshima katika
kazi zake kwa sasa amezama katika mapenzi.
Kallah
anategemea kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la You Are Not
Alone siku ya Valentine day ambao ameweza kufanya na msanii mkongwe
katika game Banana Zoro pamoja na Band yake.
Kallah
amezidi kufunguka na kumshukuru mungu kwa kazi zake kuweza kupokelewa
vizuri na jamii kiasi cha kuweza kumpa nafasi kufany6a kazi na
wasanii wakongwe katika Game kama Banana Zoro,Juma Kassim Nature na
wengine ambao yupo katika mpango wa kufanya nao kazi.
Akizungumzia
juu ya kazi yake hiyo itakayofuata baada ya walewale Kallah amesema
wimbo huo wa You Are Not Alone utazinduliwa siku ya Valentine na
utapigwa Live na Band ya B- Band ya Banana Zoro.
0 comments:
Post a Comment