MSHALE - SAGITARIUS ( NOV
23 - DES 21)
Mchana wa leo uwe na tahadhari, naona kuna taabu na
magomvi, utalaumiwa au utapata habari za ugonjwa ambazo zitakutatiza.
Wiki hii Kuna ishara ya kupata mali au fedha kutoka kwa mtu wa mbali
au kukabidhiwa mali ya watu uitunze. Lazima katika mambo yako
uwashirikishe ndugu zako ndio utafanikiwa.
MBUZI - CAPRICORN
(DES 22 – JAN 20)
Leo kuna dalili yakupata mali au kupewa pesa
au kulipwa deni lako na watu uliokuwa umewafanyia kazi siku za nyuma
ambao walikataa kukulipa. Kuna mpango wa safari uliokuwa unausubiri,
mpango huo utafunguka baada ya siku tatu kuanzia leo.
NDOO
–AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Wiki hii mtoto wako ataugua na
kuvuruga mipango yako na utavunjiwa heshima na rafiki yako ambaye
hana heshima au wewe utapata maradhi ya kuumwa na kichwa. Kuepusha
hayo safiri mbali kwa muda wa wiki.
SAMAKI – PISCES (FEB 20-
MACH 20)
Kwanza ujue kuwa safari uliyopanga kwenda ni mbaya na
yule mgonjwa yupo ndani ya shida kubwa. Ukitaka kupata mafanikio
kwanza msaidie huyo mgonjwa atoke katika matatizo yake ndio
utafanikiwa.Tegemea kuletewa zawadi kutoka kwa rafiki yako aliye
mbali.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo kuna dalili
kwamba mambo yako mengi yatafanikiwa kwa kuwatumia watu wengine bila
ya wewe mwenyewe kushiriki. Leo tegemea kukutana na mtu mkubwa
Serikalini ambaye atakusaidia au fanya mipango ya kukutana na
wakubwa.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Wiki hii
maisha yako yatakuwa mazuri, maradhi au matatizo yako madogo madogo
yatapungua. Vilevile Mkeo au mumeo atakufurahia kwa zawadi
utakayompa. Au toa zawadi kwa uwapendao mambo yako
yatafunguka.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mchana wa
leo utapokea habari za kutatanisha kuhusu kazi yako au mambo yako
ambayo yalikuwa yanakutatiza, Jaribu kuwa na subia usiyaguise mambo
hayo yanaweza kuleta matata., unashauriwa usianzishe biashara ya aina
yeyote kwa wakati huu.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Mchana
wa leo kuna kila dalili kuwa mambo yako yatafuatiliwa na watu bila ya
wewe mwenyewe kujua, jaribu kuwa mwangalifu kwa kila hatua
utakayoichukua. Kuna mtu unayemuamini sana unatakiwa uwe muangalifu
naye anaweza akakudhuru.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Mchana
wa leo kuna kila ishara ya kukwama kwa mipango yako ya kipesa,
mipango ya ndoa au mapenzi itaendelea kama kawaida, Kuna mwanamme
mrefu mweusi ukikutana naye leo au wiki hii hiyo itakuwa ni dalili ya
kufanikiwa kwa kila jambo lako.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT
23)
Leo kuna dalili kuwa mambo yako hayatakuwa safi na utahadhari
unaweza kugombana na kila mtu kazini zu kwenye biashara zako au
mtaani kwenu. Wiki hii Jitahidi kuandaa tafrija na uwakirimu watu ili
upate baraka na mikosi ikuondoke.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT
23)
Leo kuna dalili ya kuingiliwa katika kazi zako au
kusimamishwa kufanya yale uliyokuwa umeyapanga kuyafanya. Vilevile
kuna dalili ya kukimbiwa na Mpenzi wako, unashauriwa kuwa mpole na
mwenye subira ili ufanikiwe.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo naona unafikiria sana mambo ya kushirikiana na mtu katika
kazi na kipato, fanya hivyo. Ipo dalili kuwa mambo yako yatafunguka
na mikosi kuondoka. Unashauriwa usijaribu kuingia katika biashara
inayoendeshwa na ndugu yako.
0 comments:
Post a Comment