Mshambuliaji
Okwi ambaye ambaye alitua JNIA majira saa 10:04 alasiri kwa Ndege ya
Shirika la Ndege la Rwanda (Rwanda Air Ways), akiwa amevalia suruali
ya jeans na jezi ya njano yenye namba 25 kama ilivyokuwa wakati akiwa
Simba, huku mguuni akipigilia raba nyeupe na kijivu kwa juu, kabla ya
kutua na baada, jezi zake zilikuwa zikiuzwa uwanjani hapo kama
njugu.Mshambuliaji huyo alipokewa na mashabiki wachache wanaokadiriwa kufikia 200 hadi 300 tofauti na ilivyokuwa kwa Mbuyu Twite ambaye alipokelewa na maelfu ya mashabiki wa Yanga. Hali hiyo ilitokana na uongozi wa klabu hiyo kutoweka wazi mapema siku na saa maalum ambayo angetua.
Taarifa za kutua Okwi zilitolewa jana saa 7:45 mchana kupitia Kaimu Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, jambo ambalo lilichelewa kuwafikia mashabiki wa timu hiyo.
Akizunguza na waandishi wa habari, Okwi hakuwa tayari kuzungumza lolote kuhusu utata wa usajili wake zaidi ya kueleza kuwa amekuja Tanzania kufanya kazi.
"Nimekuja Tanzania kufanya kazi, safari hii kuitumikia Yanga, mambo ya usajili siwezi kuyazungumzia kwa kuwa yanahusu 'adminstration' (uongozi)," alisema.
0 comments:
Post a Comment