Thursday, December 19, 2013

BAADA YA KUANDAMWA NA SKENDO SOMA MANENO YA LULU MICHAEL HAPA

Msanii wa Filamu nchini Tanzania ambaye siku za hivi karibuni vyombo vya habari pamoja na Mitandao ya kijamii imeanza kumrudisha katika Chat ya skendo Mjini
hapa huku mwenyewe akionekana hajui wala kutambua hayo mambo yanatoka wapi.

Magazeti Pendwa yamefungua Ukurasa Mpya kwa mwanadada Lulu na kila siku kuja na Headline ya biashara ambayo inafanikisha biashara yao na kuacha maumivu kwa muhusika au ndugu jamaa wa karibu wa muhusika.

Kutokana na kutambua wazi kuwa watu wanafanya biashara kupitia jina lake mwanadada Lulu Michael aliamua kupotezea kama haoni nini watu wakiandika juu yake hali ambayo iliwafanya wahusika kutafuta namna nzuri ya wao kuweza kufanya biashara vizuri kwa kuja na Headline zinazouza zaidi na kuweza kumchafua Zaidi.

Dah nilijua mtu ukikaa kimya labda watu wanaweza kukusahau,lkn inaonekana ndo nimewapa nguvu za kuzusha na kutafuta mambo yangu kwa undani..”
haya acha tuone mwisho wake...!kama ni mm ndo natafuta Kiki au nyinyi ndo mnatafuta Kiki kupitia Mimi..!” Alisisitiza Lulu

Hebu msisahau Kama sisi wote ni binadamu...!!Inashangaza mnavyotaka tuwe na Tabia za Malaika..! Mnakwaza? Sawa mti wenye matunda ndo unapigwa mawe lkn naona huu wangu mmeamua kuujia na Lori la mawe..!na mapanga juu..!

0 comments:

Post a Comment