Msaniii anaetamba na
Ngoma yake ya 2013 ROMA MKATOLIKI ameonyesha kukatishwa tamaa na
Huduma zitolewazo na Vijana wengi katika
Makampuni,Taasisi mbalimbali
ukilinganisha Huduma zitolewazo na Watu wazima.
Sijajua
nyie mnalionaje hili wenzangu...lakini mimi naona kwa asilimia
nyingi(siyo wote) ila nyingi!!!....ya kuwa vijana wengi tunalilia na
kuhangaikia sana ajira..lakini bado hatujakuwa na wito ktk kazi zetu.
Bado
hatujakuwa na busara na hekima ktk ile kazi tunayotaka!!
na bado
tumekosa maadili katika kazi ile husika tuitakayo!!
Katika
vitengo vingi vya kazi hapa nchini, fananisha huduma atakayokupa
kijana na huduma atakayokupa mzee wa makamo/ ama mzee kabisa/mtu
mzima!!
Then umkute sista du tu binti fresh from school/ama
kijana wa kiume(brother tu) pasipo sababu yoyote anaweza akakuletea
nyodo/dharau/majigambo yani kukumbwelesha tu ili ujue bila ya yeye
huwezi fanikisha jambo lako!!
WANAKOSEA saaana!!!!
kivipi
sasa mimi nije bank/ama kwenye kampuni yako ya simu kurekebisha line
yangu ya simu!!
aaaf
eti nikunyenyekee saaana niwe muoga kwako na nikubembeleze?
wakati
wewe ndiyo unatakiwa uninyenyekee na kunibembeleza mimi mteja..maana
bila mimi kuleta line yangu hapo wewe hutapata mteja so utakufa njaa
wewe!!
na
bila mimi kuja bank kuweka pesa zangu hapo basi wewe hutapata pesa
ktk ofisi yako..sasa pesa zangu aaf still niwe mdogo mbele
yako!!?INAHUU!!
Ni tofauti na unapomkuta mzee ktk ofisi
fulani, sawa wazee wetu wana mapungufu yao lakini wengi ni wenye
busara na hekima kazini...hata majibu yao yanatia moyo na yanakufanya
ujisikie wewe ni wa muhimu!! wana uzoefu na kazi zao kwa miaka
mingi!!
Sasa sisi vijana tunalilia sana ajira na tunataka sana
tuwatoe wazee wetu ktk viti vyao walivyokalia..sawa wanakubali
kutupisha...basi tutoe huduma nzuri na inayopaswa!!
aaaf kuna
vitu vingine ukifanya wala hupungukiwi na kitu aisee tena sana sana
utaongeza urafiki na utapendwa na watu!!
Ukienda kampuni
fulani una shida fulani..aisee unaweza ukamkuta mdada akakupa majibu
hayo hadi ukajitoa thamani...
sasa nauliza mdada yule hawazi
kuwaza kuwa hata mimi nina kazi yangu...
na ipo siku anaweza
akanikuta hata mimi ni KONDA wa mbagala tandika na yeye akawa
kapoteza nauli na mimi nikaanza kumringia na ofisi yangu isiyo na
A.C!!!
kila anaekuja ktk ofisi yako siyo hohe hahe jamani kuwa
yupo yupo tu hana mchongo..ipo siku nawewe utamkuta ktk kiti chake
akikutazama kwenye foleni huku anakupania usogelee meza yake tu
uifikie AKUFURAHISHE!!!
VIJANA TUITAFTE AJIRA LAKINI
TUNAHITAJI MABADILIKO NA TUPEWE HASA SEMINA ZA MAADILI/BUSARA NA
HEKIMA KAZINI!!!






0 comments:
Post a Comment