Thursday, November 14, 2013

KOCHA STEWART HALL WA AZAM FC APATA SHAVU LA SUNDERLAND FC

Kocha ambaye alikuwa akikinoa kikosi cha Azam Fc ambaye siku za karibuni amemaliza Mkataba wake na Club hiyo na kutoendelea kuifundisha sasa atakuwa
Mkuu wa Ufundi wa akademi inayotegemewa kuanzishwa Nchini Tanzania na Kampuni ya Symbion Power kwa ushirikiano wa Sunderland FC ya England.
 
Kwa Mujibu wa Mtendaji mkuu wa Symbion Power Tanzania,Bw Peter Gathercole amethibitisha kuwa Kocha huyo aliyetoka Azam atajiunga na Akademia hiyo ambayo kwa Tanzania itakuwa na vituo viwili kimoja ni Kidongo Chekundu Sports Park na Elite Football Academy.

0 comments:

Post a Comment