Tuesday, November 12, 2013

RAY C ANAUCHUKIA MWILI WAKE SOMA ALICHOKIANDIKA JUU YA MWILI WAKE WA SASA

Alitamba kwa ngoma nyingi kali na umahiri wake wa kucheza mpaka kupewa jina la Kiuno bila mfupa Ray C.

Kutokana na mabadiliko ya maisha kwa vijana wengi Ray C kwa sasa amekuwa na Umbo kubwa kiasi ukilinganisha na enzi za Nataka kuwa na wewe Milele ambapo aliweza kuwachengua watu kibao kutokana na Swaga zileeee.

Lakini kuwa na umbo kubwa kumnampa nafasi ya kufanya mazoezi ili aweze kurejea katika hali ya kawaida ambayo mwenyewe amekili wazi wazi kuwa anaikumbuka sanaaa.

Katika mtando wa Instagram mwanadada Ray C alipost Moja ya Picha yake ya Zamani akiwa katika kazi yake iliyomfanya kupata jina la kiuno bila mfupa na kuandika maneno haya 


I miss ths sexy body!!!!Heeeeelp....I need a good trainer........!Whr r U!!!!!!”
kwa mantiki hii Ray C anachukizwa na Umbile lake la sasa hivyo anahitaji mtu ambaye atamsaidia kuondokana na mwili wake wa sasa na kurudi kule alikotoka awali.


0 comments:

Post a Comment