Huu
ni msemo ambayo alishawahi kuutumia nguli wa muzuki wa Hip Hop
Tanzania Prof Jay ambaye kwa sasa anakitumia kipaji chake kuendesha
maisha
yake na kujenga misingi mizuri ya kunufaika kutokana na kipaji
alichokuwa nacho.
Katika
kuliona suala Hili msaniii mwingine wa Hip Hop Nash Mc ambaye kwa
sasa yeye aliamua kuuza Mix Tape zake katika Mikoa mbalimbali ameamu
kuweka wazi msimamo wake kuwa hataweza kutoa nyimbo zake bure kwa
mashabiki bali kama wanakubali kazi zake wanapaswa kununua CD hizo
ili mwisho wa siku asife njaa na kipaji chake kama ambavyo imewakuta
wasaniii wengine wengi tu.
“kwa
wale washabiki wanaonitumia ujumbe ktk namba zangu,whats app wakiomba
niwatumie nyimbo zangu bure,narudia kuwaambia tena,hakuna wimbo wa
nash mc utakaopatikana bure mtandaoni,kama ktk watu 9,163
wamekosekana 2000 tu wa kununua cd zangu,bora ya kuuza kila wimbo
wangu ili nipate japo kidogo ya jasho langu”
Nategemea
kipaji changu kibadli maisha yangu na kweli kazi zinatoka cd
zinatangazwa hapa na namna zinatolewa lkn watu wanaulizia wimbo wa
bure,kama tumeshindwa kununua cd basi subiri labda nyimbo zivuje lkn
cha bure kutoka kwangu hakuna tena! Profesa jay alisema,kama una
kipaji iweje ufe na njaaa??!??
0 comments:
Post a Comment