Monday, November 11, 2013

KALA JEREMIAH ANAFUNGA MWAKA NA WALEWALE

Mwanamuziki wa Hip Hop aliyeweza kujipatia umaarufu Mkubwa na Mafanikio ya Muziki kwa mwaka 2013 Kala Jeremiah ambaye kwa sasa ni
Balozi wa Kinywaji cha Pepsi Cola amefunguka na kusema kuwa baada ya Jaribu kujiuliza na Dear God kufanya vizuri na kumpatia mafanikio makubwa katika muziki siku ya Jtano ya Week ijayo ataachia Wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Walewale ambao ametoa shavu kwa Msanii Nay Lee.

Kala amefunguka na kusema kuwa Siku hiyo ataachia Audio pamoja na Video ya Wimbo huo ili kutoa nafasi ya Watu kusikia na kuona Ujumbe uliowasirishwa katika Ngoma hiyo ambayo huenda ikiwa na ngoma ya mwisho kwa Kala Jeremiah kutoa kwa Mwaka huu 2013.

0 comments:

Post a Comment