NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo unaweza kusamehewa iwapo utakuwa inajisikia vibaya na huwezi
kutekeleza majukumu yako,kuwa mkarimu kwako mwenyewe na kwa watu
wengine na usifanye jambo lolote ambalo hulipendi, na kwa kufanya
hivyo hata ikibidi ujifungie chumbani kitandani kwako fanya
hivyo.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
.Usikubali
mtu yoyote akuchokoze, umeshaelezea hisia zako na umeshawasikiliza
watu hisia zao. Kuna watu wanataka kupambana na wewe lakini wewe
unajihisi kwamba una amani ndani ya moyo wako. Shirikiana na marafiki
zako walio karibu leo jioni.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN
20)
wapenzi watakujia kwa wingi wiki hii, na katika hao utaweza
kupata mmoja ambaye utakuwa nae kwa muda mrefu. Hao wengine unaweza
ukafurahi nao kwa muda. Kati ya hao kuna wengine pamoja na kukutaka
urafiki watakuwa sio wazuri.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR
28)
Kipindi hiki inaonekana matatizo yameshaanza kukuandama,
inaonekana unaanza kuchanganyikiwa kutokana na mzigo wa matatizo
ulionao. Unajua kabisa kwamba kuna majukumu ambayo unatakiwa
uyatekeleze lakini hujayafanyia kazi. Unashauriwa kwamba yatekeleze
hayo majukumu haraka sana itakusaidia kuondokana na shida.
SAMAKI
– PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kuna mambo ambayo yanakushinda
kuyaingia na kuyatekeleza, fanya subira utagundua mengi yaliyofichika
katika hayo.ikiwezekana jaribu kuyaacha na uwe mtulivu kuna mengi
mazuri yako njiani yanakuja.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR
20)
Kuwa muangalifu sana iwapo mtu yoyote atataka umshauri katika
jambo lolote. Unaweza ukawa mtego ambao utakutumbukiza katika
matatizo. Kwa hivi sasa jitahidi kujiepusha na kujiingiza katika
jambo lolote na utafute njia ya kujitoa iwapo umo katika mpango au
mradi hasa wa kifedha.
NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY
20)
Wiki hii utapata kazi au mpango mzuri wa kifedha ambao
utakukwamua kutokana na matatzizo ya ghafla yaliyokufika. Mtafute
rafiki yako mpendwa na mpelekee kilio chako, atakusikiliza na
kukusaidia. Mamb yako karibu kufunguka kuliko unavyofikiria.
MAPACHA
- GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo una shughuli nyingi sana za kufanya
na hiyo kazi unayoifanya inahitaji nguvu bidii na akili kuikamilisha.
Unatakiwa ujikakamue ili uweze kuikamilisha vinginevyo utapata
matatizo.washirika wako watakufurahia ukiikamilisha. Ni vyema
ukamshirikisha huyo unayemfikiria kwa sasa.
KAA - CANCER (JUN
22- JUL 22)
Jambo lolote lililokuwa linakutia wasiwasi hapo
awali, ikiwa ni masuala ya fedha, mambo ya hisia au kazi suluhisho
litakujia kiajabu ajabu. Utagundua ghafla njia ya kukufanya uondokane
na matatizo hayo na itafanyika bila ya kumuudhi yoyote. Wote
wanaokuchukia watafurahi.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Bado
mawimbi ya wasiwasi yanakuandama lakini kwa vile sasa ule uzito
umepungua umepumzika kidogo na watu wanakufurahia sana, Jaribu kukaa
nyumbani, pumzika na tafuta ushauri. Hakuna njia nyingine.
MASHUKE
– VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama ikiwa kazi zako zinahusisha
watoto au ukiwa una watoto wako mwenyewe, jihadhari na tabia yako
mbaya. Mmoja wa watoto hao anaweza kukuumbua kwa kutoa siri zako kwa
watu. Hiyo inaweza kukuletea balaa.
MIZANI – LIBRA (SEPT 24-
OCT 23)
Leo utapata furaha ya kukutana na rafiki yako wa zamani
au mshirika wako. Kama akikutaka akununulie chai au kahawa au chakula
nenda wala usisite kwa sababu kuna habari atakupa na zitakusaidia
sana kukubadilisha kimaisha.
0 comments:
Post a Comment