Friday, November 8, 2013

HIKI NDICHO ALICHOSEMA DJ AD MAFUVU Baibeeeeyyy

Dj ambaye anafanya poa sana katika Radio na Tv  Dj AD Mafuvu ambaye anahusikika katika vipindi mbalimbali vya Radio na Tv katika Ting'a Namba
moja kwa Vijana EATV amefunguka ya moyoni juu ya Shirika moja la Serikali na kusema kuwa linakoelekea linataka kuwapeleka wananchi litakavyo.
 
Mkali huyo ambaye aliweza kuwapagawisha wananchi katika Show mbalimbali za Kili Music Tour 2013 zilizofanyika katika Mikoa Mbalimbali leo amefunguka katika Ukurasa wake wa Facebook kama hiviiii.

daaaaaaah! hawa tamesco sasa wanakoelekea watatushika mpaka makalio, yaani gharama hizi za umeme bado wanataka kupandisha eti kwa kuwa kuna sheria inawalinda ambayo inawapa mwanya wa kupandisha tozo kila baada ya miaka 3. huu si utoto sasa!”
Hivi serikali yetu kwanini isiwape nafasi watu wakaleta mitambo ya ufuaji umeme bila kutozwa ushuru wa kuingiza hiyo mitambo? hivi haiwezi kusaidia kweli???
hawa tamesco tangu miaka ya giza huko wapo tu wanazingua! watoe nafasi kwa gharama za chini au bila ghalama kwa wananchi wenye uwezo wa kuleta mitambo ya ufuaji umeme tuondokane na hii sijui tuite opareshi vimbwanga vya tamesco!
shirika liko lenyewe nchi nzima miaka nenda miaka rudi na linatoa huduma muhimu na inayohitajika kwa wananchi, lakini cha ajabu mpaka leo linashindwa kujiendesha sawa sawa na kutoa huduma yenye kukidhi viwango na hitaji la wateja wake!!!??
sasa mnafanya nini kwenye hizo nafasi mlizokaa??? mnazingua sana nyie jamaa! tazama upande wa mawasiliano, watu wangapi hapo ulipo wanatumia titisiemo kwenye huduma za simu zao za mikononi??? yaani ingebaki hii titisiemo nahisi mpaka leo hizi huduma tunazopata tungezipata miaka hamsini ijayo.
sio kama nawadiss, ila mashirika mengi ambayo yanamkono wa serikali mnazingua sana, mnajali maslahi yenu binafsi tu!!! mnatuzingua sanaaaaaaaa, mnatuchosha na utendaji wenu m'bovuuuuuuuuu !!!



0 comments:

Post a Comment