Msanii wa nyimbo za Injili Tanzania Bahati Bukuku ambaye siku za karibuni
amempoteza Baba yake mzazi, ameeleza kusikitishwa na kifo
hicho cha
baba yake mzazi .
Bahati Bukuku
amedai kuwa , mzazi wake huyo amekufa kimaajabu alipokuwa amelazwa
kwenye Hospitali ya Dokta Mvungi iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Bahati alisema kuwa
baba yake hakuugua ila alipata presha iliyosababishwa na mshituko
uliotokana na kupewa taarifa ya mdogo wake aitwaye Gibbons kupigwa
risasi.
“Hakika baba
yangu amekufa katika mazingira ya kushangaza sana, alipata taarifa
kwamba mdogo wake Gibbons alipigwa risasi, akapata presha, akaugua
ini na kuanzia hapo hakuamka tena mpaka mauti yalipomfika.
Source:Global
Plublisher






0 comments:
Post a Comment