11:49 PM

NGE-SCORPIO
OKT 23-NOV 21:
Unatakiwa kuwa mwangalifu sana, kosa dogo tu
linaweza kukusababishia kupoteza vitu vyako vya thamani au kujikuta
umo kwenye kesi ambayo hukuitegemea kuipata.
MSHALE-SAGITTARIUS
NOV. 22-DES 20:
Jihadhari na watu utakao kutana nao katika vyombo
vya usafiri au safarini, kwani wengine si wema kwako. Tegemea
kukutana na mtu mkubwa au maarufu katika safari zako.
MBUZI-CAPRICON
DES 21-JAN 18:
Unatakiwa kuwa mwangalifu sana katika shughuli
zako, pia jitahidi kutochanganya masuala ya kazi au biashara na
mapenzi, kukaribisha hali hiyo ni kukaribisha
kufilisika.
NDOO-AQUARIUS JAN 19-FEB 18:
Mambo yako mengi
yatakunyookea, unatakiwa kujiepuesha na majungu na fitina za watu.
Kuwa mkarimu kwa watu wote watakao kujia na shida zao.
SAMAKI-PISCES FEB 19-MACH 20:
Siku nzuri kwako kwani yale
magonjwa na kesi zilizokuwa zikikukabili utashinda, usikubali kutenda
kosa lolote kwa kumfurahisha mtu, kwani kufanya hivyo ni kujitafutia
kifungo cha aibu.
PUNDA-ARIES MACH 21-APR 20:
Malumbano
yeyote utakayoyafanya na wakubwa zako yatakupotezea kazi yako.
Unatakiwa kuwa mpole kwa kila kitu utakachoambiwa na wakubwa
zako.
NG’OMBE-TAURUS APR 21-ME I20:
Wiki hii utapata
kazi nyingi zitakazo kuingizia pesa nyingi. Utapeli hautakuacha
mbali, kuwa makini na kila hatua unayoichukuwa
MAPACHA-GEMIN
MEI 21 - JUNI 20:
Leo utapata barua au salamu za kukupongeza kwa
kazi nzuri uliyoifanya hivi karibuni. Tegemea kupokea wageni kutoka
kwenu watakao kuletea habari muhimu. Mpenzi wako atakufurahisha
sana.
KAA-CANCER JUNI 21-JULAI 20:
Usipende kurukia mambo
usiyoyajua au yasiyo kuhusu. Unashauriwa kuwa usipende kutumia nguvu
kwa kila jambo. Waone wazee kwa ushauri zaidi kabla ya kuamua jambo
lolote.
SIMBA-LEO JULAI 21-AGOSTI 21:
Leo mambo yako
yatakunyookea na kipato chako kuongezeka, mambo ya mapenzi au unyumba
yatakuwa ya kufurahisha. Mpenzi wako mpya atakusaidia katika kazi
zako.
MASHUKE-VIRGO AGOSTI 22-SEPT 22:
Shughuli zako
ulizokuwa unazifanya hapo awali zitaanza kutoa matunda. Fitina zote
ulizokuwa unafanyiwa zitashindwa na wewe kuibuka mshindi. Pendelea
kufanya ibada na kutoa sadaka.
MIZANI-LIBRA SEPT 23-OKT 22:
Ni siku nzuri kwako kuyashughulikia matatizo yote yanayoikabili
familia yako, kabla ya kuyashughulikia matatizo ya kikazi. Mambo ya
mapenzi si ya kuyafuatilia sana au kupoteza muda wako.
0 comments:
Post a Comment