Tuesday, October 15, 2013

:YANGA WATAKIONA CHA MOTO-JAMHURI KIHWELU :TUTAWASHANGAZA SIMBA-YANGA

Zikiwa zimebakia siku Tano kwa watani wa Jadi Simba na Yanga kukutana katika Uwanja wa Taifa siku ya Jumapili watani hao wameaanza kupeana tambo za hapa na pale.

Wakati  mabingwa wa ligi kuu ya Bara, Yanga jana walitua kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Simba.

Wekundu wa Msimbazi wao wamehamisha kambi kutoka Bamba Beach na kwenda Bagamoyo.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro jana alifunguka kwa njia ya Simu na kusema kuwa kikosi chake kiliwasili Pemba jana kwa ajili ya kambi hiyo.

Alisema timu hiyo imeamua kupiga kambi visiwani humo ili kukwepa usumbufu, ikiwa ni pamoja na kutaka kuwapa wachezaji nafasi ya kufanya mazoezi kwa uhuru zaidi tofauti wanapokuwa Dar es Salaam.
 
"Timu iko vizuri, wachezaji wote wanaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo," alisema na kuongeza kuwa wanatarajia kuwashangaza Simba.

Alisema wachezaji wote sasa wako poa baada ya majeruhi wa muda mrefu Salum Telela naye kurejea mazoezini.

Kwa upande wa Simba Kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema jana kuwa Simba ambayo imekuwa kambini Bamba Beach, Kigamboni imehama mahala hapo na kwenda Bagamoyo jana jioni. 

Julio alisema Yanga watakiona cha moto katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.

0 comments:

Post a Comment