Hata
hivyo, Mhavile alisema kwamba yeye siyo msemaji wa familia isipokuwa
naye amekwenda hospitalini hapo kumwona mfanyakazi wake baada ya
kusikia tukio hilo, kwani hakuwapo nchini, lakini hali yake ni nzuri
kwani Ufoo sasa anawatambua watu wote wanaokwenda kumwona.
“Hali yake kwa kweli ni nzuri, naweza kusema anaendelea vizuri, ingawa mimi siyo msemaji wa familia, lakini ana kumbukumbu kwani anawatambua watu wote, anazungumza na hata maswali anayoulizwa anaweza kuyajibu, kwa kweli anaendelea vizuri,” alisema Mhavile.
Mhaville alisema kwa kuwa upasuaji ulichukua muda mrefu, madaktari wameshauri kuwa mtangazaji huyo anahitaji saa 72 za kupumzika na baada ya hapo ndipo watafanya tathmini ya maendeleo yake.
NIPASHE ilimshuhudia Mtangazaji huyo akiwa amelazwa kwenye chumba binafsi kwenye jengo la moyo, huku ndugu wa karibu pamoja na wafanyakazi wenzake wachache wakiruhusiwa kuingia na kumwona ili kumpa nafasi ya kupumzika.

Ufoo
alijeruhiwa vibaya kwa risasi alfajiri ya Oktoba 13, huku Mama yake
Mzazi akiuawa kinyama na Mzazi mwenzie Ufoo, Anthery Mushi, baada ya
kile kinachodaiwa ni ugomvi wa wawili hao uliosababisha waende kwa
mama yake Ufoo eneo la Kibamba CCM nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam kwa lengo la kuwasuluhisha.
Baada ya kumuua Mama yake Ufoo, Bibi Anastazia Saro, kisha kumpiga Ufoo risasi mbili, naye alijipiga risasi ya kidevu kuelekea juu iliyosababisha kifo chake.
Ufoo alikimbizwa Hospitali ya Tumbi na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanyiwa upasuaji kwa zaidi ya saa sita ili kuondoa risasi mwilini mwake.
Afya ya Ufoo ikizidi kuimarika, habari za kiuchunguzi kutoka watu wa karibu na Mushi zinasema kuwa miaka miwili iliyopita alitaka kuteketeza nyumba waliyokuwa wanaishi na Ufoo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam, lakini jamaa zake waliingilia kati na kumzuia kabla ya kufanya uhalifu huo.
Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa kwa ujumla Mushi alikuwa ni mtu mkimya asiyesema sana, kiasi kwamba kujua kwa uhakika nini anawaza ilikuwa ni vigumu.
Watu walio karibu naye wanasema kuwa ingawa kukaa mbali na Ufoo kwa muda mrefu kunaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa mahusiano kati yao, inaelezwa kuwa alirejea nchini Alhamisi iliyopita kimyakimya na kukaa Dar es Salaam kwa siku moja.
Kesho yake, yaani Ijumaa Mushi anadaiwa kuwa alikwenda Moshi kijijini kwao, Uru Mawella, kumwona mama yake mzazi.
Alikaa Moshi na kurejea Dar es Salaam Jumamosi, na kesho yake Jumapili ndipo alichukua maamuzi hayo ya kinyama ya kumuua mama mkwe, kumjeruhi mzazi mwenzake akijua amekwisha kumuua na kisha kujiua mwenyewe

Habari za kipolisi zilizotolewa juzi
zilisema kuwa begi la marehemu Mushi lilikuwa na vifaa hatari ikiwa
ni pamoja na bastola ambayo anamiliki kihalali, kisu kirefu, shoka
dogo, pingu moja, kamba na mifuko miwili mikubwa inayosadikiwa ni ya
kuhifadhi maiti.
Wapelelezi wa Polisi waliokataa majina yao kutajwa gazetini kwa kuwa siyo wasemaji wa polisi, walisema kulingana na madai ya ndugu kuwa marehemu Mushi aliingia nchini kimya kimya na kwa zana alizokutwa nazo, ni kama alikuwa amepanga mpango wa mauaji mapema, ama kumuua Ufoo na mtu mwingine ambaye haijulikani.
“Inawezekana hii ni premeditated killings. Unakuaje na silaha zote hizi kwa wakati mmoja halafu haya yatokee,” alisema askari huyo akiasa jina lake lisitiriwe.
Juzi Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa siri ya janga lote hilo anayelijua kwa undani ni Ufoo mwenyewe.
Katika hatua nyingine, kaka wa marehemu, Silva Mushi, jana alisema amestushwa na msiba wa mdogo wake huyo kwa kuwa hakuwa na taarifa ya kuwasili kwake nchini.

Alisema taarifa ya msiba alipata kupitia vyombo ya habari zilipokuwa vikitangaza tukio hilo la kusikitisha, lakini kama vyombo hivyo visingetoa taarifa haikuwa rahisi kwake kujua tukio hilo.
“Sijawahi kupata taarifa kama kulikuwa na ugomvi baina ya Ufoo Saro na marehemu mdogo wangu, hivi sasa tumekusanyika hapa kupata nauli ya kusafirisha mwili wa marehemu Alhamisi wiki hii,” alisema.
Mushi alisema ikiwa mipango na mikakati ya mazishi itaenda vizuri, wanatarajiwa kusafirisha mwili kwenda kuzika katika eneo la Uru kijiji cha Ongoza, Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro siku ya Ijumaa.
Wakati huo huo, mwili wa mama yake Ufoo Saro unatarajiwa kusafirishwa leo kupelekwa Machame Shari, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika kesho.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi hayo, Allelia Swai, mipango yote imekamilika, ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha Polisi kwa ajili ya maziko hayo.
Swai alisema kuwa kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi watauchukuwa mwili wa marehemu kutoka Muhimbili na kuupeleka nyumbani Kibamba kwa ajili ibada ya kuagwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), lililopo mtaa wa Kibwegere.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment