Mkali wa Hip Hop
anayewakilisha jiji lenye miamba mingi Mwanza,Young Killer Msodoki
amefunguka na kusema kuwa ametimiza ndoto yake jana baada ya kufanya
kazi na Msanii mkongwe katika Fani ya Bongo Fleva Dully Sykes.
Killer amefunguka na
kusema kuwa Dully skyes ni msanii aliyekuwa anamkubali na kumshabikia
tangu zamani wakati hajui kama atakuja kuimba.
Kazi zimefanyika ndani
ya studio ya 4:12 ya Dully Sykes na kutayarishwa na Dully mwenyewe.
“Kwanza kabisa
namshukuru Mungu kwa kuwa ndiye muweza wa yote, jana tulikuwa na
project yetu na Dully, kwanza kabisa picha linaanza mimi ni shabiki
mkubwa sana wa Dully. Dully kaanza muziki wakati niko shuleni na
sijui hili wala lile, kwa hiyo nilikuwa na dream kubwa sana kuja
kufanya kazi na bro Dully na jana bahati nzuri mwenyezi Mungu
amebariki tumefanya kazi, haijalishi kama itatoka leo au kesho..na
sidhani kama itaishia kazi hiyo, tunaweza kufanya kazi nyingi na
nyingi zaidi.” Amefunguka Young Killer.
0 comments:
Post a Comment